Bwana Keddy Abubakari Mgumia na Bi. Sabrina Haji Mmanga wamefunga ndoa katika hafla iliyofanyika tarehe 16 Agosti 2026 jijini Dar es Salaam.
Sherehe hiyo ilifanyika kwa furaha na bashasha, huku ikihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza kusherehekea siku hiyo muhimu katika maisha ya wanandoa hao.
Katika hafla hiyo, Keddy na Sabrina walipokea pongezi pamoja na salamu za heri kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki, wakiongozwa na dada yake Keddy, Mwandishi wa Habari na Mhariri, Sidi Abubakari Mgumia.
Ndugu, jamaa na marafiki wanawatakia Keddy na Sabrina ndoa yenye upendo, amani, furaha, baraka na mafanikio katika safari yao ya maisha ya ndoa.
Hongereni sana Keddy na Sabrina! Tunawatakia maisha mema na yenye furaha katika ndoa yenu.

Comments
Post a Comment